Saturday, April 19, 2014

SIKU YA KUKUTANA NA WAPENZI WOTE WA JAYDEE KUSHEREHEKEA MUZIKI WETU

Tickets za VIP ni sh. 50,000/=
Ambapo utapata dinner na wine mezani.

Tickets zingine ni sh. 20,000/= kwa siti za wapenda ku dance kama mimi.

Nunua yako mapema kuepuka usumbufu
Zinapatikana Nyumbani Lounge, Shear Illusions Mlimani City na Million Hairs SALON

Kwa bookings za meza tafadhali piga namba 0787 630 459
Historia Concert ni tar 2 May 2014
Pale pale kwenye parking zetu - Nyumbani Lounge
Karibu uonyeshe ushirikiano

Zitapigwa zote uzipendazo kuanzia Machozi, Hazigandi, Distance Yahaya mpaka Nasimama
Live na Machozi Band

Tuesday, February 4, 2014

Monday, February 3, 2014

LUNCH YA LEO JUMATATU - NYUMBANI LOUNGE - VITAKUWEPO VYAKULA HIVI NA VINGINE VINGI

Ni kuanzia saa 6:00 mchana mpaka saa 10:00 jioni
Fresh juice, soda, na maji na WiFi ni bure
Utafaidi utamu kama uzuri wa picha unavyojionyesha

Monday, December 30, 2013

DIARY YA LADY JAYDEE - JUMAPILI YA TAR 5 JANUARY 2014.... SAA 3:00 USIKU EAST AFRICA TV

Nilizaliwa nyumbani na sio hospitalini kama watu wengine
Na ndani ya nyumba hii ndimo nilizaliwa
wazazi wangu walikuwa wanaishi hapa, kwenye nyumba ya kupanga
Maandalizi mema ya kuupokea mwaka.

nitakachowaletea kipya mwaka 2014 
ni story za kutia moyo na kufariji
usikose kuchungulia Diary yangu 
kila siku za Jumapili saa 3:00 usiku
EATV PEKEE

Marudio huwa ni kila Jumatatu saa 8:00 mchana na Alhamis saa 4:00 usiku

Wednesday, December 18, 2013

MWAKA UNAISHA UMETIMIZA MALENGO / NDOTO YAKO AU BADO UNAOTA?

 Dr. Dre

Usher Raymond

Miaka inaweza kuwa inaenda halafu una ndoto nyingi, hata ikapita miaka 10, 20 au hata mpaka 30 na malengo yako ukawa hujatimiza lakini bado ukawa hukati tamaa
Nilitamani kumuona Whitney Houston lakini mpaka anakufa sikufanikiwa hilo.....
Nimefanikiwa vitu vingi sana na vikubwa 2013, lakini nakiri kuna ndoto sijazitimiza na bado naziota kila siku.

Kati ya NDOTO zangu mbili kubwa zilizobakia hapa duniani ni kukutana na watu hawa wawili
Dr. Dre na Usher Raymond
2013 hiyoooo inayoyoma ndoto imekuwa ndoto, hebu tusaidiane kusali tujaribu tena 2014.

NDOTO yako wewe ni ipi??? Kila kheri na kwako pia katika kuzikimbiza na kuzitimiza ndoto zakoHABARI ZA CHRISTMAS


Kila tunapopita ndio picha na taa tunazoziona zinang'aa mitaani
Ni msimu umefika na unakaribia kuisha
Zikiwa zimebaki siku tu kadhaa kabla ya kuhitimisha sikukuu kubwa ya christmas
Wewe umejipangaje?? Ya kwako utaisherehekea wapi??


Ni vizuri kusherehekea sikukuu na watu uwapendao.
Sisi tunakupenda, na wewe kama ni mmoja wa watu unaependana na sisi basi karibu tusherehekee kwa pamoja tukipeana faraja na mawazo mbali mbali
Tar 24 Dec 2013 ni mkesha wa Christmas Lady JayDee na Machozi Band tutakuwepo NYUMBANI LOUNGE kukupatia burudani mbali mbali, muziki, vinyaji na chakula kitamu
Hii ni kwa watu wazima wenye umri kuanzia miaka 18 na kuendelea
Siku ya Tar 25 Dec 2013 Mchana kuanzia saa 8 mchana - saa 3 usiku ni party maalum kwa ajili ya watoto
Ni zamu yao kuonyesha vipaji na kufurahi, ni watoto watoto na watoto wazazi pia mnakaribishwa kuambatana nao, ili nao wapate nafasi yao kuburudika

Karibuni sana

Wednesday, December 11, 2013

Wednesday, December 4, 2013