Friday, May 4, 2012

BIRTHDAY YA SHY-ROSE BHANJI @NYUMBANI LOUNGE

 Birthday girl mbunge mteule wa Afrika mashariki Shy-Rose Bhanji akiwa na keki yenye rangi za CCM
 Shy-Rose akiwa na marafiki zake Mh. Vicky Kamata, Mh. Catherine Maige & William Malecela
Wabunifu wa mavazi Asya & Mustafa pia walikuwepo 
 Mh. Halima Mdee na Cake ya CCM, kama ushoga sawa ila kwenye itikadi hata!
 Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano kwa Tiketi ya Chama cha Mapinduzi waliangua Vicheko pale wenzao wa CHADEMA walipoikwepa kuigusa nakuila Keki ya Birthday ya Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki Shy Rose Banji wakati wa tafrija yake iliyofanyika Nyumbani Longe Jijini Dar es Salaam. 

Wabunge hao wa CHADEMA  ni Halima Mdee (Kawe) ambaye anaonekana picha ya juu akiikataa keki hiyo iliyotolewa na Wakurugenzi wa Nyumbani Longe, Gadna G Habash na Mkewe Lady Jay Dee, huku Mbunge wa Viti Maalum, Lucy Kiwelu picha ya chini nae akijificha asiitazame kwa karibu.

Wabunge hao waliigwaya Keki hiyo kutokana na jinsi ilivyopambwa rangi za CCM.

Huku Wabunge wa CCM wakishangilia wakimtaka Halima Mdee aongoze Ukataji wa Keki hiyo ambayo ilitolewa baada ya keki ya awali iliyoandaliwa na Baby Girl Shy Rose kuliwa, ilishindikana kuliwa na kuhifadhiwa.

Watu mbalimbali walihudhuria tafrija hiyo ndogo wakiwepo Wabunge, wanasiasa, Wasanii musiki, Watangazaji na Wanahabari ambapo kila aliye simama kuongea alimpongeza sana Shy Rose kwa kuwa Mpambanaji wa Ukweli katika kutafuta kile anachotaka na kumuombea kwa Mungu amuongoze vyema katika kazi yake. (habati hii kwa hisani ya Mrokim)
 Mh Zitto Kabwe nae alikuwepo
 Birthday girl akifurahi na wageni wake
 Wasanii wa Bongo Flava pia walikuwepo
Fid Q pamoja na Jaffarai, pembeni DJ Venture
 Ile idara yetu iliwakilishwa ipasavyo na shem wangu Cathbert Kajunason
 Time to pop
 Cheers
 Msanii Linah Blanche akitoa burudani
Birthday girl akiongea machache
Picha kwa hisani ya Michuzi, MrokiM & Kajunason blogs

Copied from: Jestina G Blog

8 comments:

Anonymous said...

TUKO PAMOJA DAIMA!

Jamani Waheshimiwa Wabunge wetu mmeonyesha mwamko wa hali ya juu wa Kuchanganyika pamoja kama ndugu moja licha ya 'kuwa Mzungu wa nne Kiitikadi' hapo mimi kama Mwananchi wa kawaida nimefarijika na nimefurahi saana!.

Lakini MHE. HALIMA MDEE, MHE. LUCY KIWELU na MHE. ZITTO KABWE kuandaliwa Keki ya Rangi ya CCM/ YANGA na Uongozi wa Mjengoni 'Nyumbani Lounge' kwa ajili ya Birth day ya Mpendwa wetu Mbunge Mteule Baby Girl 'SHY ROSE BHANJI,,,KULA AU KUONA KEKI HIYO SIO DALILI YA KUWA MMEHAMIA 'CHAMA TAWALA' CCM AMA MMESAJILIWA KWA DIRISHA DOGO KWA UHAMISHO KUTOKEA KLABU YA MSIMBAZI HADI KLABU YA JANGWANI!,,,Wala msiogope,,,HIZO NI RANGI ZA KEKI TU!

Anonymous said...

Jamaniieee kipendacho roho hula nyama mbichi !

Yaaani keki ya 'kijani na njano' taaaamuuuuu kweli kweli!

Mpo hapo Mhe. Mdee, Mhe.Zitto na Mhe. Kiwelu?

wise monica kaaya said...

Hahahahahaha apo pa cake ya ccm pamenifurahisha sana awakutaka kusaliti chama chao jamani goood happy birthday babegirl nakuombea maisha marefu tupiganie vyema mamy

Anonymous said...

KEKI:

Mhe. Lucy Mhagama na Mhe. Halima Mdee mngewaweza kwa kuileta keki kwa siri, kuwapa kukata Keki ktk giza taa zizimwe hapo sehemu ilipo keki halafu baada ya kukata ziwashwe na kushuhudia wameshakata keki ya C.C.M !

Ohhh hilo lingekuwa BAO LA MWAKA !

Anonymous said...

Hahahaa 100% Keki nia ya C.C.M aka YANGA !

Kombe mmeshachukua mwaka huu 2012 na pia Baraza la Mawaziri mmeshalibadili.

Na keki yetu CCM/YANGA pia muikatae?

Twawaongoza lakini Assalama Leko zenu CHADEMA na MSIMBAZI !

Upo Mhe. Zitto Kabwe?

Anonymous said...

Ni kweli Mdau kazi wameifanya Chadema/Simba kulazimisha mabadiliko ya Mawaziri na kuchukua Kombe.

Lakini sawa kataeni keki yetu CCM aka YANGA isipokuwa ushindi wenu ni wa ZAWADI TU,,,mmepata kwa bahati na 'mipango' Kombe 2012,,,au mnabisha? sasa kwa Taarifa yenu Msimbazi aka Chadema hata kama mmebadili Mawaziri na Kombe mnalo sisi YANGA aka CCM kesho tunawafunga!

Anonymous said...

BAO LA MATOKEO YA MPIRA KESHO:

YANGA SC-78: SIMBA SC-0

Sisi Yanga kwa ghadhabu ya kulikosa Kombe pamoja na ninyi kuikataa keki yetu ya Birthday tutawafunga idadi kubwa ya 'Mabao' sawa na mwaka wa kuzaliwa yaani 1978 kama mnavyoona bao la matokeo litakavyosoma Dakika ya 91 (Yaani dakika 1 baada ya Mwamuzi kupuliza Filimbi na Mpira kuisha kesho)

PATAKUWA NA PART MBILI:

1.JANGWANI/ na Mjengoni 'NYUMABNI LOUNGE' :::::SHEREHE ZA KUIFUNGA SIMBA SC MABAO 78 !

2.MSIMBAZI/:::::SHEREHE ZA UBINGWA 2012 !

JE, NAULIZA MNIJUZE NI NANI KATI YA NO. 1 AMA NO. 2 ATAFURAHI AKICHEKA HUKU AMENUNA?

Anonymous said...

Hahahahahaha !

Jamani niacehni nichekeee !

Mhe. Shy Rose sawa sawa Keki ya Rangi hiyo inawafaa wakataji wawe Mhe. Halima Mdee na Mhe. Lucy Kiwelu !

Halafu walaji muhimu Mhe. zitto awe mmoja wapo au siyo?

Msiogope hamna 'Limbwata' la CCM hapo !

Ni maadili yetu Watanzania ukichinja Jogoo mkubwa na wali wa mchele mpya unamwalika na kumkirimu mwana ndugu ale ubwabwa kwa minyama nyama !