Saturday, May 5, 2012

MATEMBEZI YA KUANGALIA VIFAA BORA VYA MUZIKI VITAKAVYOFAA KUTUMIA SIKU ZA USONI


Mbali na kuuza na kununua Piano
Allen & Fisher pia wanazi service zile zinazohitaji matibabu, wana kusanya Pianos mbalimbali zilizowahi kutumiwa na watu maarufu miaka ya nyuma.

Na ambazo wao wanaamini zina kiwango cha hali ya juu ukilinganisha na Piano nyingi zinazotengenezwa miaka ya sasa, ambazo zinang'aa juu ila utumbo wa ndani umeoza

Au zinang'aa juu utmbo wa ndani ni plastic ikikatika haina replacement...Tunaziita za Mchina
Ila kwa sura ukiziangalia unaingia mkenge

Katika tafuta, tafuta tulipita kuangalia baada ya kujuzwa kuwa kuna wataalam wa maswala hayo mjini Cape Town.

Inaitwa window shopping.
Ni vema kufanya hiyo window shopping kwanza sehemu mbili tatu, ili usije paramia mzigo wa kichina siku mbili tatu halilii, Mara linakoroma kama chura.
Tulikuwa na mwenyeji wetu alieongoza msafara Donald Korosso (bonge ya mtu) na Captain G akiwa mtathmini viwango, Jide ni testa wa kubofya bofya

Hiyo Piano inayoonekana hapo juu kwenye picha ina jina la Rud-Ibach-Sohn
Hili kubwa linajulikana kama GRAND PIANO
Ndogo yake inaitwa BABY GRAND
Rud-Ibach-Sohn ni brand ilioanza miaka ya Alfu moja mia nane naa, (sisi tushaga zoea tu YAMAHA, YAMAH).
Utumbo wake wa ndani unatengenezwa kwa kutumia Rose Wood ni kifaa toka Germany

Ukigusa zile buttons zake ukanyanyua kidole kusogeza kwenye button nyingine, mlio unakuwa bado unaendelea kuskika, very tricky.
Kwa beginner kama mimi.

Ila ni mzigo ambao ukiutwaa utakutwa na yoyote atakaekuja kuutumia huko mbele ya safari.
Kwa mujibu wa maelezo tuliopewa na wahusikwa waliopo kwenye workshop ya Allen & Fisher Piano

Kwamba tukiutwaa huo tunaouwezo wa kuutumia miaka 40-50 ijayo bila kuufanyia service ya aina yoyote

Na bei ya hilo kubwa unaloliona kwenye picha hapo juu ni sawa na shillingi za kitanzania milioni 40.

Kwa mimi kama ningekuwa nazo, bora hilo Piano kuliko nguo na viatu vya Designers.....Maana nikilipata hilo ni mtaji wa kunirudishia hizo Mil.40 na zaidi ya hapo
Kwa kifupi hicho ni kitegauchumi.

Manake kama linadumu miaka 40-50
Hiyo mil.40 itakuwa haijarudi tu miaka yote hiyo???
Isitoshe wanakuhakikishia kukurekebishia pale linapopatwa matatizo ndani ya kipindi flani tangu ununue kwao
Kijana mwenye jacket la blue ndio alikuwa kitoa maelezo hayo, lakini pia anapiga Piano vizuri sana
Maana huwezi kufanya kazi sehemu inayouzwa kifaa hicho kama hujui kujaribishia wateja wanaokuja kuwa kinaliaje...........

Wateja pia kama mnajua kupiga mnaruhusiwa kujaribu

Piano zinaletwa kufanyiwa service hapo
Pia wanauza na ku tune Pianos mbali mbali
Na material ya ndani ni mbao pamoja na sponji laini
Ambayo hata ikiharibika au kupinda inakuwa rahisi ku fix, (ku replace) Tofauti na Plastic

Hizi ni baadhi ya Piano zilizoletwa kutibiwa kwenye work shop hiyo.
Mbali na kufanya service na kuuza pia wanaweza kukubadilishia rangi, kwa mfano umenunua Piano nyeusi, na ungependa rangi nyeupe wanakupakia rangi unayotaka.


 
Mizigo yote imefunikwa kwa Blanket kuzuia vumbi na purukushani nyinginezo zinazoweza kuleta madhara kwa vifaa hivyo

Humu ndani ni sehemu ambayo kuna mafundi
Na hili Piano moja ndio liko kwenye wakati wa kubadilishwa

Linasubiriwa likauke warudishie utumbo wa ndani
Limebadilishwa kutoka rangi ya kawaida ya ubao na kuwa jeupe.....

Ukitaka pia wakubandikie jina lako (Custom made)
Mfano libandikwe LADY JAYDEE badala ya YAMAHA
Wanaweza fanya hivyo, ila unalipa hela ya ziada


Kama umevutiwa na maelezo haya
Unahitaji kuwasiliana nao, kila kitu kimeandikwa hapo kwenye hiyo kadi..............

Wanakuletea mpk ulipo kama uko Cape Town
Kama unalitaka kwa Tanzania wanafanya mipango ya usafiri ila utaulipia mwenyewe.

Kwa kipindi hiki mazungumzo yangu ni Piano tu, mpaka hapo litakapotokea jingine jipya
Week end njema
 

14 comments:

Subi Nukta said...

Very informative and useful post.
Shukurani Jide.
Nawe pia wikiendi njema na window shopping njema.

(Swali la kiuchokozi, leo YNWA tunakung'utana nanyi Blues kwenye mtandange wa FA, mtachomoa? Ngoja tuone mi tayari nipo mbele ya skrini nasubiria kuona mta'vyokimbizwa mchaka mchaka, usikimbie tu kijiwe tukikukung'uteni leWo nhe he...)

Anonymous said...

Dada nakukubali natamani kuwa nawasiliana nawe unipe mbinu za kufanya biashara. nurumagreth@yahoo.com

Nuru said...

Big up my sister. I like u. Ukipata nafasi tupe na sisi mbinu za biashara. nurumagreth@yahoo.com

Anonymous said...

Nakukubali. naomba unisaidie ujasiliamali. nurumagreth@yahoo.com

wise monica kaaya said...

Mungu akujalie uchukue ilo unalopiga litarudisha mkwanja tena ndani ya mwezi tu all da best mamy

Anonymous said...

Nabado uefa

Subi Nukta said...

Leo mmetukimbiza, hongereni Chelsea! Wacha nikusubirieni Munich, mi nitakuwa Bayern, tuwemo!

Jide said...

Pole sana Subi ndio game ilivyo. Karibuni tena siku nyingine.@Nuru tafadhali niandikie e-mail au tuwasiliane nikirudi kwa namba 0767 884007. Karibu tubadilishane mawazo.

Subi Nukta said...

Kushapoa mie leo nime-walk alone wacha tu nikalalaGE nikimbiaGE na warusha madongo, mwe.

Ester Ulaya said...

thinking yako Jide naikubali, najua unaelewa namaanisha nini, Nice Post

stevie-u.s said...

Jide kwa ushirikiani captain naamini mtakamata chombo kikali cha kukonga nyoyo za wapenzi.

cisca kayumbo said...

nimekumis mamii warudi lini jamanii nataka kuja tena kukuona

diadora said...

Hongera najua utanunua hilo la miaka 40. Kwa imani kila kitu kinawezekana. Mungu aliekuwezesha kufanya maajabu huko nyumba ndie huyo huyo hajabadilika.

happy happy said...

amaizing!